Hawa ni baadhi ya wabunge wanaotuhumiwa kwa Ruswa kutoka kamati zao za bunge.
Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge
wanaotajwa kuvuliwa nyadhifa zao wakati
wowote kutokana na tuhuma za RUSHWA ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini,
Martha Mlata ambaye ni Mbunge wa Viti
Maalumu (CCM), i Mwenyekiti wa Kamati ya
Uwekezaji na Mitaji (PIC), Richard Ndassa,
ambaye pia ni Mbunge wa Sumve (CCM) na
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na
Mazingira, Dk. Mary Mwanjelwa ambaye ni
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) pia wamo
Makamu wenyeviti Dk. Raphael Chegeni (Kamati
ya Huduma za Maendeleo ya Jamii) ambaye pia
ni Mbunge wa Busega (CCM), Mbunge wa
Mwibara, Kangi Lugola (CCM), Kamati ya Hesabu
za Serikali za Mitaa (LAAC), Mbunge wa
Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilaly (CCM), ambaye
ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za
Serikali (PAC).
Taasisi zilizotajwa kutoa RUSHWA ni Shirika la
Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC), Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya (NHIF) na Mamlaka ya Udhibiti wa
Huduma za Nishati na Maji (Ewura) ambapo kila
mmoja wa wajumbe wa kamati anatuhumiwa
kupokea kuanzia kiasi cha Sh milioni nane.
Uchunguzi umeonyesha kwa mfano Kamati ya
Huduma ya Maendeleo ya Jamii ilimtuma katibu
wake ambaye ni mtumishi wa Bunge kwenda
kuchukua mzigo wa kamati hiyo katika ofisi za
NHIF, lakini alipofika alikabidhiwa MFUKO WA
SANDARUSI uliojaa fedha ambazo alikataa
kuzipokea. Ofisa huyo ambaye anatakiwa apewe
nishani ya juu kabisa ya jamhuri ya muungano
kwa kukataa RUSHWA alirudi na kuitaarifa
kamati hiyo kwamba ameshindwa kuchukua
mzigo huo kwa sababu ni mfuko wa SANDARUSI
wenye fedha jambo ambalo haruhusiwi kwa
mujibu wa tararibu na kanuni za kazi zake.
Hii ni tabaia ilijengaka na wabunge hawa tangu
enzi ya utawala wa msoga, na kufanya tabia ya
wizi na rushwa kuota mizizi na hali masharika
yetu ya umma yakifa kwa sababu ya wizi
uliokubuhu., Ningepena ili iwe fundisho kwa
wabunge wengine serikali iwavue ubunge wao na
kufungwa miaka 50 jela iwapo watakuwa
wamejihusisha na vitendo hivi, kuwavuwa nyazifa
zao siyo haki kwani huku ni kuvunja miiko ya
ubunge na kuhujumu uchumi wa nchi.chanzo gazet la nipashe.
0 comments :
Post a Comment