Watoto wawili wa familia moja wafariki dunia na baba yao kujeruhiwa baada ya moto kuunguza nyumba.
Watoto wawili wa familia moja wamefariki dunia
huku baba yao akijeruhiwa vibaya na kulazwa
katika Hospitali teule ya wilaya ya Muheza
kufuatia nyumba yao kuteketea kwa moto baada
ya mafuta ya Petrol yaliyokuwa yamehifadhiwa
katika nyumba hiyo kulipuka.
Wakizungumza katika eneo la tukio lililopo kijiji
cha Songa mama mwenye nyumba iliyoteketea
kwa moto pamoja na mashuhuda wa kijiji cha
Songa Batini kilichopo kata ya Songa wilayani
Muheza,wamesema moto huo umesababisha vifo
vya watoto wawili wenye umri wa miaka 4 na 5
waliokuwa wakicheza ndani ya nyumba hiyo
ambao wamefahamika kwa majina ya Mariam
Zubeir,Neema Zubeir ambao wamefariki dunia na
baba yao Zubeir Athuman ambaye amelazwa
katika hospitali teule ya wilaya ya Muheza
akiendelea na matibabu.
Akielezea jinsi walivyofanya jitihada za kuuzima
moto huo ili kuokoa maisha ya watoto hao,mzee
wa kijiji aliyeshiriki kuuzima moto huo Aweso
Bakari amesema walilazimika kutumia maji ya
msikitini ili kuokoa maisha ya watoto hao lakini
bahati mbaya walifunikwa na bidhaa zilizokuwa
zikiteketea kwa moto.
0 comments :
Post a Comment