Haya ni maamzi magumu aliyo yafanya Rais uhuru kenyatta kenya.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametaka
kukamatwa kwa mmiliki wa nyumba ilioanguka
mjini Nairobi na kuwaua watu saba.
Kenyatta aliyezuru mkasa wa tukio hilo pia
amewataka wakaazi wa nyumba zilizopo karibu
na eneo hilo kuondoka wa kuwa nyumba hizo
zimethibitishwa kutokuwa salama.
Maafisa wa Kaunti ya Nairobi wamethbitisha
kuwa nyumba hiyo ilikuwa imeorodheshwa
miongoni mwa majumba yaliotarajiwa kuvunjwa
kwa kuwa haikuafikia viwango vya nyumba ya
kuishi watu wengi.
Juhudi za uokoaji zinaendelea lakini zimetatizwa
na mvua kubwa inayoendelea mbali na uwezo wa
kufikia eneo hilo.
Jeshi la Kenya linaloongoza juhudi hizo za uokozi
limelazimika kutumia mikono na misumeno ya
kielektroniki kuchimba chini ya vifusi kwa kuwa
vifaa vinavyohitajika katika zoezi hilo haviwezi
kuingia katika eneo hilo.
0 comments :
Post a Comment