Klabu ya Barcelona imekili kukabiwa na ushindani LA LIGA
Klabu ya Barcelona italazimika kushinda mechi
zake zote za mwisho ili kushinda taji la ligi ya
La Liga kwa kuwa huenda wapinzani wao
wasipoteze hata pointi moja kulingana na kocha
Kuis Enrique.
Viongozi Barcelona walioanza mwezi wa April
wakiwa na pointi nane kileleni mwa ligi hiyo,wako
sawa kwa pointi na Atletico Madrid huku Real
Madrid ilio nafasi ya tatu wakiwa nyuma kwa
pointi moja.
''Haiwezekani kwamba timu zilizo nyuma yetu
zitapoteza pointi'',alisema Enrique siku ya
Ijumaa.
''Mchezo wetu ni mzuri katika kipindi hiki cha
mwisho''.
Barcelona iko mbele ya Atletico kutokana na
tofauti ya mabao.
Barca,Atletico na Real Madrid zote zinacheza
Jumamosi katika muda tofauti.
KIabu ya Zinedine Zidane inaweza kwa masaa
machache kupanda katika kilele cha ligi iwapo
itashinda dhidi ya Real Sociedad katika mechi ya
mapema.chanzo bbc.
0 comments :
Post a Comment