Kijue kilichompata mwenyekiti wa halmashauri ya kibondo .soma zaid.
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kibondo, Simon Kagoli amefikishwa
mahakamani kwa kosa la kuhifadhi
wahamiaji haramu nyumbani kwake na
kuwatumikisha mashambani.
Kagoli ambaye pia ni Diwani wa Kata ya
Kageji, anakabiliwa na mashitaka matatu
ikiwemo kuishi na watu ambao sio raia,
kuwasaidia raia wa kigeni kutenda kosa
na kuajiri na kuwatumikisha wageni
shambani mwake.
Kesi hiyo namba 114/2016 iko mbele ya
Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Kibondo,
Robert Male.
Mwendesha Mashitaka wa Uhamiaji,
Richard Mwangole alidai mshtakiwa
alitenda kosa hilo kwa makusudi huku
akijua kuwa kuhifadhi wahamiaji haramu
ni kosa kubwa.
Anatuhumiwa kuwafanyisha kazi
wahamiaji hao na kuwalipa ujira wa Sh
110,000 kila mmoja. Male alikana makosa
na yuko nje kwa dhamana.
Alidhaminiwa na wadhamini wawili, kila
mtu kwa dhamana ya Sh milioni moja.
0 comments :
Post a Comment