Breaking News
Loading...

Advert

Monday, April 25, 2016

Wazir proff.muhongo ataja sababu kubwa zilizofanya bomba la mafuta kutoka uganda mpaka tanga tanzania.soma zaid.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo amewasili nchini kutoka Kampala,
Uganda na kusema miundombinu ya Tanzania na
usalama wake ni moja ya mambo yaliyowezesha
Tanzania kupata dili la ujenzi wa bomba la
mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi bandari ya
Tanga.Akizungumza na waandishi wa habari
mara tu baada ya kuwasili jana jioni alisema
kwamba maunganiko ya reli ya Tanga hadi reli ya
Kati na uwapo wa barabara kumeipatia Tanzania
nafasi ya ujenzi wa bomba hilo kwani kaskazini
mwa Kenya miundombinu hiyo haipo.
Akizungumza huku akimfagilia Rais John
Magufuli kwa kazi yake nzuri ya kusimamia
ujenzi wa barabara wakati alipokuwa Waziri wa
Ujenzi, alisema kama kungelikosekana
miundombinu hiyo kungeliikosesha Tanzania
mradi huo muhimu Afrika Mashariki.
Tanzania ilikuwa inashindana na Kenya katika
kupata nafasi ya kutekeleza mradi huo wenye
kilomita 1,403 utakaobeba mafuta ghafi kutoka
Hoima nchini Uganda hadi Tanga. Mradi huo wa
dola za Marekani bilioni 4 sawa na Sh trilioni 8.7
ni ushindi mkubwa kwa Watanzania ambao
walipeleka Uganda timu ya wataalamu
kuwezesha ushawishi.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top