Breaking News
Loading...

Advert

Monday, April 25, 2016

Ripoti ya CAG yaibua madudu mengi.soma zaidi.

=> Ulaji na uzembe vinatajwa kubeba
sehemu kubwa ya ripoti hii.
=> Misamaha ya kodi 2014/15 ni asilimia
2 ya pato la taifa kinyume cha asilimia 1
=> Halmashauri 40 hivi ndo zenye hati
safi kati ya halmashauri zaidi ya 160
=> Bidhaa a bilioni 9 za kupelekwa nje
ziliuzwa hapa hapa nchini. Upigaji huo wa
ukwepaji kodi.
=> Bidhaa za bilioni 89 za nje hakuna
ushahidi kama zilienda Rwanda, Burundi
na Uganda.
=> Rufaa za kodi nyingi mno zimedoda
mahakamani na hivyo kuikosesha serikali
kodi
=> Deni la Taifa hadi Juni 2015 lilifikia
trilioni 33.5. Ndani ya mwaka mmoja
lilikua kwa trilioni 7!
=> Malipo kwa deni kwa mwaka ni trilioni
4.
=> Deni na mishahara inamaliza mapato
yote ya taifa. CAG anahoji, tutapata wapi
pesa za maendeleo?
=> CAG Anataka maduka ya fedha za
kigeni yadhibitiwe
=> Vyama vya siasa, kimoja tu
kimewasilisha hesabu. Vyama 21 bado,
Msajili afiatilie. Hajakitaja chama
kilichowasilisha
=> Mishahara hewa katika Taasisi za
umma 16 ni Shilingi bilioni 390.
Mishahara ambayo haikulipwa na
haikurejeshwa hazina ni bilioni 2
=> Sh. Milioni 700 za makato ya
watumishi kwa Katavi na Kilimanjaro
hayakuwasilishwa kwenye mifuko ya
Hifadhi ya Jamii.
=> Sh. Milioni 827 za vifaa vya upigaji
kura zilitumika kwa kazi isiyo na tija
katika Uchaguzi 2015
=> Nakala 158,003 za Katiba Pendekezwa
hazikusambazwa kwa walengwa wakati
wa mchakato wa Katiba Mpya
=> Manunuzi yenye thamani ya Sh. Bilioni
27 yalifanywa na Mashirika ya Umma bila
ushindani
=> Cheti cha uendeshaji ATC kimeisha
muda tangu 2010. ATC ina Wafanyakazi
wengi kuliko kazi zilizopo
=> Bidhaa za bilioni 9 za kupelekwa nje
ziliuzwa hapahapa nchini. Nia ni kukwepa
kodi!
=> Bidhaa za Sh. Bilioni 89 za kwenda nje
hakuna ushahidi kama zilienda Rwanda,
Burundi na Uganda.
=> CAG ataka UDA irejeshwe serikalini.
Mwenyekiti wa Bodi ya UDA, Idd Simba
aliwekewa sh. milioni 320 ktk akaunti
yake binafsi.
=> Kampuni ya SAAFI inadaiwa Sh. bilioni
17. Hii ni ya mwanasiasa mkongwe,
Mzindakaya.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top