Kinondoni yabain watumishi hewa wapya 55.
Bado agizo la Rais wa awamu ya tano wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John
Pombe Magufuli la kuwatoa katika mfumo wa
mishahara watumishi hewa linazidi kushika kasi
kila kukicha, leo April 28 2016 mkuu wa wilaya
ya Kinondoni Ally Hapi amethibisha kuongeza
kwa idadi ya watumishi hewa.
Wilaya ya K inondoni imebaini watumishi hewa
wapya 55 baada ya uchunguzi wa awali kubaini
watumishi hewa 34 pekee, sasa mkuu wa wilaya
ya Kinondoni amethibisha rasmi kuwa wilaya ya
Kinondoni imefikisha jumla ya watumishi hewa
89, watumishi hewa wa kwanza 34 walikuwa
wanaitia serikali hasara ya zaidi ya milioni 500.
“Katika mambo ambayo mkuu wa mkoa aliniagiza
niyafanyie kazi wakati nateuliwa na Rais ni
watumishi hewa, nimekuta taarifa ya watumishi
hewa 34 ambao walikuwa wameisababishia hasara
serikali ya zaidi ya Tsh milioni 512, nilivyoteuliwa
kuwa mkuu wa wilaya wiki moja iliyopita
nimelifanyia kazi na kubaini watumishi hewa wapya
55” >
0 comments :
Post a Comment