Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, April 28, 2016

Mkuu wa wilaya kigoma apiga apiga stopu nyumba ya urithi kubomolewa.


Kigoma. Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Savery
Mwangasame amesitisha uvunjwaji wa nyumba
ya urithi baada ya kubaini kuwa taratibu za
uuzaji wake zilikiukwa bila kuwashilikisha
wanafamilia kwa kutumia hati ya kughushi.
Uamuzi wa mkuu huyo wa wilaya umefanyika
katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, baada ya
wanafamilia hao kutolewa mali zao zote nje ya
nyumba wanayoishi na polisi jamii kwa agizo la
mahakama kuwa, tayari imeuzwa.
Akizungumza na wanafamilia hao, Mwangasame
amesema, amesitisha uvunjwaji huo hadi
ufafanuzi utakapotolewa baada ya mazungumzo
na makubaliano kati ya familia hiyo na
msimamizi wa mirathi.
“Nimeagiza zoezi hili lisitishwe mpaka hapo
uhakiki wa hati na vigezo vingine vya uuzaji wa
nyumba hii utakapofanyika na familia nzima
kuridhia uuzaji huo,” amesema Mwangasame.chanzo mwananch.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top