Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, April 28, 2016

Rais john magufuli ametengua uteuzi wa mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji nchini(TIC).soma zaid

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji
nchini (TIC),Bi.Juliet Kairuki.
Taarifa iliyotolewa na kwa vyombo vya habari na
katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji, Prof.
Adolf Mkenda, imesema kuwa hatua hiyo imekuja
baada ya rais Magufuli kupata taarifa kuwa
Mkurugenzi huyo alikua hachukui mshahara wa
serikali tangu alipoajiliwa mwaka 2013 hatua
ambayo rais amezua maswali mengi.
Aidha Taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu
huyo imeongeza kuwa endapo Bi. Kairuki
atakuwa tayari kuendelea kufanyakazi na Serikali
ya awamu ya tano atapangiwa kazi nyingine huku
mchakato wa kumpata Mkuregenzi mpya
umeanza mara moja.
Kwa mujibu wa Prof. Mkenda kwenye taarifa
yake hiyo amesema Bw. Clifford Katondo
Tandali, atakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji
wa kituo hicho cha uwekezaji nchini TIC.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top