Mechi ya costal unioni na yanga imeshindikana kumalizika uwanja wa mkwakwani.siam zaid.
Mchezo huo umevunjika katika dakika ya 105
huku Yanga ikiongoza kwa mabao 2-1.
Coastal Unioni ndiyo waliokuwa wa kwanza
kupata bao dakika ya 54 kupitia kwa Yussouf
Sabo aliyefunga kwa shuti kali nje ya 18, huku
mabao ya Yanga yakitiwa kimiani na Donald
Ngoma dakika ya 60 na Amis Tambwe dakika ya
95.
Awali dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo
kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1,
ambapo kwa mujibu wa kanuni za mashindano
hayo, imebidi dakika 30 ziongezwe, ambapo
katika dakika ya 95 Amis Tambwe aliifungia
Yanga bao la 2.
Kadri muda ulivyokuwa ukisonga mbele, licha ya
hali ya giza kutanda uwanjani, hali ya usalama
ilikuwa ikizidi kuwa tete kutokana na mashabiki
wa Coastal kuonekana kutoridhishwa na
uchezeshaji wa waamuzi wa mchezo huo.
Mashabiki na wapenzi wa Coastal walikuwa
wakilalamikia magoli yaliyofungwa na Yanga kwa
madai kuwa goli la Kwanza lililofungwa na
Ngoma, halikuwa halali kutokana na mfungaji
kuwa ameotea kabla ya kufunga.
Pia bao la pili lililofungwa na Tambwe
limelalamikiwa kwa madai kuwa mfungaji kabla
ya kufunga aliunawa mpira.
Katika hatua nyingine mwamuzi alimzawadia kadi
nyekundu nahodha wa Coastal Adeyum Ahmad
baada ya kushika mpira kwa makusudi katika
muda wa ziada baada ya Tambwe kufunga bao la
pili.
Baada ya kadi hiyo mpira ulisimama kwa muda
kutokana na wachezaji na mashabiki wa Coastal
kutoridhishwa na maamuzi ya mwamuzi, na hivyo
kusababisha mwamuzi kuahirisha mchezo huo,
ambapo haikufahamika mara moja sababu za
kuahirisha mchezo huo.
Akizungumzia hali hiyo, kaimu mkurugenzi wa
mashindano wa shirikisho la soka TFF, Jemedari
Said amesema kuwa mchezo huo umevunjika
kutokana na vurugu zilizozuka uwanjani hapo na
kwamba TFF inasubiri ripoti ya msimamizi wa
mechi ili kufanya maamuzi.
0 comments :
Post a Comment