Walimu kuchangia gharama za mwenge Tanga.
WAKATI utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano
ukijinisabu kwamba, umejipanga kupunguza
makali ya maisha kwa wananchi, kwa Jiji la
Tanga mambo hayapo hivyo, anaandika Regina
Mkonde.
❝
Halmashauri ya Jiji hilo imepeleka ujumbe
kwa walimu wote jijini humo kuchangia pesa
kwa ajili ya kugharamia mbio za Mwenge.
Mwisho wa kupokea michango hiyo ni tarehe
25 Aprili mwaka huu.
Ujumbe wa barua hiyo umeandikwa na Gwakisa
Lusajo kwa niaba ya Dk. Wedson Sichalwe,
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga.
Barua hiyo imeelekeza kwamba, kila mwalimu
anayefanya kazi kwenye jiji hilo anapaswa
kuchangia Sh. 1,000 ambapo walimu wakuu kila
mmoja ametakiwa kutoa Sh. 10,000.
Pia imeelekeza kuwa, pesa hizo zipelekwe kwa
Rehema Said, Mratibu wa Mwenge wa Wilaya ya
Tanga.
MwanaHALISI Online umemtafuta Sichalwe ili
kujua uhalali wa walimu kuchangishwa fedha kwa
ajili ya mbio za Mwenge jijini humo.
Sichalwe amekiri kutambua barua hiyo ya kuhitaji
michango kutoka kwa walimu na kudai kwamba,
ni jambo la hiyari.
“Lazima watu wajue kuwa, barua iliyotolewa
haikuwa na lengo la kushinikiza watu watoe
michango hiyo. Ni hiyari ya mtu, na ndiyo maana
tulitoa kwa wadau mbalimbali ikiwemo sekta
binafisi na kampuni,” amedai Sichalwe.
Anasema, muhusika atakayepokea michango
atatakiwa kutoa stakabadhi ili kuwahakikishia
wachangiaji kwamba, fedha zao hazitatumiwa
kinyume na makubaliano.
“Vile vile, haimaanishi kwamba ni michango ya
fedha tu ndiyo inapokelewa, bali hata mwenye
vifaa ambavyo vitasaidia kufanikisha shughuli
yetu tunavipokea, kwa mfano mafuta ya gari na
vyakula,” anasema.
Hata hivyo, Sichalwe ameshindwa kutoa
ufafanuzi kuwa, kama ni mchango wa hiyari
kwanini alipanga viwango vya kutoa kwamba,
walimu wakuu watoe Sh. 10,000 na walimu wa
kawaida watoe Sh. 1,000.
Amedai, michango hiyo ni kwa ajili ya ununuzi wa
mahitaji ya wageni siku ya tukio ikiwemo chakula
na mafuta ya gari kwa ajili ya usafiri.
Ametaja tarehe ya siku ambayo Mwenge
utapokelewa jiji humo kuwa ni tarehe 4 Mei 2016
katika Uwanja vya Tunda Ua vilivyopo kwenye
Kata ya Kilale na kwamba, tarehe 5 Mwenge
utapelekwa visiwani Unguja.chanzo mwanahalisonline.
0 comments :
Post a Comment