Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, April 23, 2016

Pombe yawaponza saa za kazi wawekwa rumande huko serengeti mara.soma zaid

Mkuu wa Wilaya Sengerema, Zainabu Terack
alitoa amri ya kukamatwa na kuwekwa mahabusu
watu hao juzi baada ya kukuta baa
zimefunguliwa huku wakiendelea kupata kinywaji
kabla ya saa 9.30 alasiri ambao ndiyo muda wa
kufunga ofisi za umma.
Sengerema. Wilaya ya Sengerema mkoani
Mwanza imeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la
Rais John Magufuli kwa kuwasweka rumande
watu wanane waliokutwa wakinywa pombe baa
wakati wa saa za kazi.
Mkuu wa Wilaya Sengerema, Zainabu Terack
alitoa amri ya kukamatwa na kuwekwa mahabusu
watu hao juzi baada ya kukuta baa
zimefunguliwa huku wakiendelea kupata kinywaji
kabla ya saa 9.30 alasiri ambao ndiyo muda wa
kufunga ofisi za umma.
Serikali imepiga marufuku unywaji wa pombe,
mchezo wa pool na michezo mingine wakati wa
saa za kazi kama mkakati wa kuhakikisha kila
Mtanzania anashiriki shughuli ya uzalishaji mali
katika eneo lake.
Terack aliongoza operesheni hiyo kwa dakika 45
kusaka wanywa pombe na wacheza pool muda
wa kazi.
Watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa
mahakamani kwa tuhuma za uzembe na kukiuka
amri halali ya Serikali kwa kunywa pombe saa za
kazi.
Wakijitetea baada ya kutiwa mbaroni, baadhi ya
waliokutwa wakinywa pombe muda wa kazi
ambao hawakutaka kutaja majina yao walidai
walikwenda katika baa hiyo kujiliwaza kwa msiba
wa ndugu yao, Petro Shoyo na kumuomba mkuu
huyo kuwasamehe kwa sababu ni kosa lao la
kwanza na hawakukusudia kukiuka agizo hilo.
Utetezi na ombi hilo haukufua dau mbele ya
mkuu huyo baada ya kusisitiza watuhumiwa hao
wawekwe mahabusu na kuchukuliwa hatua ili iwe
fundisho kwa wengine.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top