Breaking News
Loading...

Advert

Friday, April 29, 2016

Shule ya skondari Bomani tarime toka ianzishwe 2012 haina mwalimu wa somo physics


Tarime. Tangu ianzishwe mwaka 2012, Shule ya
Sekondari Bomani iliyopo Kata ya Bomani
wilayani Tarime mkoani Mara, haina mwalimu wa
fizikia.
Licha ya kuwa hivyo, wanafunzi katika shule hiyo
wanalazimika kufanya mtihani wa kidato cha nne
wa somo hilo.
Mkuu wa shule hiyo, Samsoni Agai amesema
kutokana na mpango wa Serikali wa kutoa elimu
bure, huenda ukaathiri masomo ya sayansi kwa
madai awali wazazi walikuwa wakichanga fedha
kuwalipa walimu waliokuwa wakijitolea
kufundisha masomo ya sayansi kutoka nje ya
shule hiyo.
“Lakini baada ya kupiga marufuku michango,
hatuna fedha za kuwalipa na imebidi walimu hao
wasitishe kufundisha,” amesema mwalimu huyo..
Mwanafunzi wa kidato cha pili, Bhoke Marwa
amesema Serikali inapaswa kuajiri walimu wa
sayansi, kwani upungufu uliopo unasababisha
mwanafunzi kufeli masomo hayo.chanzo mwananch.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top