Breaking News
Loading...

Advert

Friday, April 29, 2016

Siri ya Utumbuaji majipu hapa nchini wafichuka.soma zaid.


ALIYEKUWA Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh,
amefichua siri ya Rais Dk. John Magufuli
kutumbua majipu kwa kasi, tangu ameingia
madarakani mwaka jana.
Akizungumza wakati wa kuzindua ripoti mbili za
Mpango wa Uhamasishaji Uwazi katika Mapato
ya Madini, Gesi na Mafuta (TEITI), mjini Dar es
Salaam jana, Utouh alisema akiwa CAG aliandaa
ripoti nyingi ambazo utawala uliopita
haukizifanyia kazi.
Alisema Rais Magufuli anatumia ripoti hizo
kutumbua vigogo mbalimbali, kwa sababu
amekuta mambo yako mezani.
“Ripoti zangu nikiwa CAG ndizo zinasomwa
bungeni, zimeonyesha udhaifu maeneo
mbalimbali ya taasisi za Serikali na nyingine.
“Nyingi zilikabidhiwa zamani,viongozi waliopita
hawakuzifanyia kazi…nawaambua utumbuaji
majipu unaofanywa na Rais Magufuli, utasaidia
kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato na nidhamu
sehemu za kazi.
Alisema ni jukumu la kila mwananchi kulinda
rasilimali zilizopo na kwa kufanya hivyo, mapato
yataongezeka.
Kuhusu sheria ya madini iliyopitishwa mwaka
jana, inayozungumzia uwazi na uwajibikaji katika
sekta ya madini, Utouh alisema imesaidia kuleta
nidhamu katika sekta hiyo, kwa sababu kabla ya
hapo mapato mengi yalikuwa yakipotea.
Naye Mwenyekiti wa TEITI, Jaji Mark Bomani
alisema taarifa za kazi za TEITI katika ripoti ya
mwaka 2013/14, zimesaidia kunufaisha
uhamasishaji uwazi katika sekta ya madini
nchini.
Alisema sekta hiyo ilianza kushamiri mwaka
1990, haikuwa na manufaa kwa uchumi wa nchi
kwa vile mapato kwa Serikali hayakuwa wazi.
Alisema mwaka 2007, Rais mstaafu, Jakaya
Kikwete aliunda kamati ya kuchunguza sekta ya
madini ambayo kwa miaka mingi ilikuwa
ikilalamikiwa na wadau wengi.
Alisema upotevu wa fedha za Serikali mwaka
2009, zilikuwa hazionekani, lakini CAG Utouh
alifanya ukaguzi ambao umesaidia fedha za
madini kuongezeka.
“Ripoti ya mwaka 2014 inaonyesha pato katika
sekta hii, limeongezeka kwa asilimia 10…takwimu
zetu zinaonyesha awali kampuni za madini
zilikuwa 11, sasa zimefika 60 zikiwamo kubwa na
za kati,”alisema.
Utouh alistaafu rasmi kazi Septemba 2014, baada
ya kuitumikia nafasi hiyo kwa miaka saba
alipoteuliwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete
mwaka 2006.chanzo mtanzani.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top