Ufisad UEFA polisi wavamia ofsi kwa uchunguzi.
Afisi za shirikisho la soka barani Ulaya Uefa
zimevamiwa na maafisa wa polisi wa Uswizi
baada ya aliyekuwa katibu mkuu Gianni
Infantino ambaye sasa ni rais wa Fifa kutajwa
katika stakhabadhi zilizofichuliwa na kampuni
moja ya mawakili wa Panama Mossack Fonseca.
Imebainika kwamba Infantino alikuwa mmoja ya
watu watatu waliotia saini kandarasi za haki za
kupeperusha moja kwa moja matangazo ya
mechi za vilabu bingwa Ulaya runingani mwaka
2006.
Watu hao wawili ambao ni wafanyibiashara
wametuhumiwa na madai ya kutoa hongo
Infantino hatahivyo amekana kufanya makosa
yoyote.chanzo bbc swahili.
0 comments :
Post a Comment