Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, April 6, 2016

Afrika ya kusini kufanya uchaguzi wa majimbo agosti 3.2016

Uchaguzi wa majimbo ya Afrika Kusini
utafanyika Agosti tarehe 3 mwaka huu.
Rais Jacob Zuma alitangaza tarehe hiyo siku
moja tu baada ya kuponyoka kura ya kutokuwa
na imani naye bungeni iliyokuwa ikiongozwa na
vyama vya upinzani kufuatia kupatikana na hatia
ya ubadhirifu wa mali ya umma na matumizi
mabaya ya mamlaka yake na mahakama ya juu
zaidi nchini Afrika Kusini.
Rais Zuma anasema nia yake kuu ya kuitisha
uchaguzi huo wa mashinani mapema ,ni
kutathmini umaarufu wa chama chake cha ANC
kufuatia tuhuma kuwa amepoteza uhalali wa
kuiongoza taifa hususan baada ya kupatikana na
hatia ya kupuuza maamuzi ya mahakama ya
taifa hilo.
Zuma aliwataka wenyeji wajiandikishe kuwa
wapiga kura kwa wingi iliwathibitishie upinzani
kuwa kweli Afrika kusini imekomaa kidemokrasia.
Wanaomkosoa wanasema ndie kiongozi asiye na
umaarufu kwa wote tangu taifa hilo lijinyakulie
uhuru wake mwaka wa 1994 na wanamtaka
ajiuzulu.
Hii leo vyama vya kupigania haki za kibinadamu
visivyo vya kiserikali vimejiunga na wale
wanaomtaka ajiuzulu wadhfa wake vikisema
amepoteza uhalali baada ya uamuzi huo wa
mahakama ya juu.
Wengine waliomkaripia rais Zuma na kumtaka
ajiuzulu ni aliyekuwa jaji wa mahakama ya juu
Zac Yacoob, balozi mstaafu wa Afrika kusini
nchini Uingereza Cheryl Carolus, kiongozi wa
vyama vya wafanyikazi Zwelinzima Vavi kwa
mujibu wa jarida la News24.
Katika tukio la kushangaza, Tawi la chama
tawala cha ANC cha jiji la Johannesburg,
kimemtaka Zuma ajiuzulu.
Tawi hilo ndilo linalokabiliwa na ushindani
mkubwa zaidi kutoka upinzani kwani wenyeji
wake wamekuwa wakiwasikiza sana viongozi wa
upinzani wakiongozwa na Julius Malema wa
chama cha EFF.
Hata hivyo matawi mengine ya chama tawala
ANC, ikiwemo lile la wanawake na pia la vijana
yangali yanamuunga mkono rais Zuma.
Zuma amekiri makosa yake na amekubali kulipa
fedha zote zilizotumika kufanyia ukarabati
makaazi yake ya Nkandla.chanzo bbc swahil.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top