Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, April 12, 2016

Ufisadi wa billion 1.7 halmashauri wa babati.soma zaidi.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Dr Joel Bendera
amevitaka vyombo vya dola mkoani humo kuanza
kufanya uchunguzi wa tuhuma za matumizi
mabaya ya fedha ya mradi wa upimaji na uuzaji
wa viwanja kwenye shamba la katani la Maisaka
lililopo mjini Babati unaowahusisha Maafisa saba
wa halmashauri hiyo akiwemo aliyekuwa
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji huo Bw.Omari
Mkombolwa kwa tuhuma za kumsababishia
mwajiri wao hasara ya shilingi bilioni 1.7
Akisoma taarifa hiyo mbele ya kamati ya ulinzi
na usalama ya mkoa huo na wilaya,wananchi na
wakuu wa idara mbele ya baraza maalum la
halmashauri ya mji huo kabla ya kukabidhi taarifa
ya kamati ya uchunguzi kwa TAKUKURU, na
Polisi Dr.Bendera amesema amezingatia azimio
la baraza la halmashauri hiyo la oktoba 30,2014
na kuunda kamati maalum kufuati kuwepo kwa
malalamiko mengi ya wananchi waliokosa
viwanja ilhali wakiwa wamelipia.
Hata hivyo Dr.Bendera amesema baadhi ya
watuhumiwa wamehamia halmashauri nyingine
amevitaka vyombo hivyo kuwatafuta ikibidi
kuwakamata ili kuwarudisha kujibu tuhuma
zakutoa zabuni kwa kampuni zisizosajiliwa,bodi
ya zabuni kupuuza kwa makusudi sheria ya
ununuzi,kugawa viwanja vingi kwa mtu
mmoja,ubadhilifu na kula njama na
wakandarasi,manunuzi hewa na kughushi
stakabadhi na mihuri feki akasisitiza wakithibitika
wafikishwe mahakamani.
Kwa upande mwingine Mbunge wa Jimbo la
Babati Bi.Pauline Gekul licha ya kueleza
kuridhishwa na kamati hiyo kwa kuwahoji
watuhumiwa hao huku hatua inayofuata ikiwa ni
kutoa nafasi kwa vyombo vya dola kufanya
uchunguzi,lakini ameomba mamlaka husika
kulihoji baraza la madiwani kwani kumekuwepo
na mkanganyiko wa takwimu.
Wanaohusishwa na tuhuma hizo ni aliyekuwa
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bw.Omari
Mohamedi Mkombolwa, Afisa mipango Hamisi
Massaka, Mwanasheria Bw.Reginald Mtei,
Mhandisi Mathias.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top