Breaking News
Loading...

Advert

Friday, April 8, 2016

Wanao tuhumiw kwa ufisadi wakataliwa dhamana.

Korti ya Kisutu leo yakataa kuwachia
Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya
sambamba na Waliokuwa Wafanyakazi wa
Benki ya StanBic Tanzania, Sioi Sumari na
Shose Sinare kwa kuwa mashtaka yao
hayana dhamana.
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU), tarehe 1/4/2016
iliwafikisha Mahakamani aliyekuwa
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania na Mwenyekiti wa ‘Enterprise
Growth Market Advisors Ltd’ (EGMA), Bw.
Harry Msamire Kitilya; aliyekuwa Mkuu wa
Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji wa
Benki ya Stanbic Tanzania, Shose Mori
Sinare pamoja na Aliyekuwa Mwanasheria
wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Sioi
Graham Solomon.
Washtakiwa wote walishtakiwa kwa
makosa ya:- Kula njama na kujipatia kwa
udanganyifu kinyume na kifungu Na. 384
cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E.
2002) ; Kughushi kinyume na kifungu Na.
333,335 (a) na 337 cha Kanuni ya
Adhabu (Cap 16 R.E 2002) ; Utakatishaji
wa fedha haramu kinyume na kifungu Na.
12 (a) 13 (a) cha Sheria ya ya
Utakatishaji fedha Na. 12 ya Mwaka 2006
‘Anti- Money Laundering Act’.
Hiki kimbunga kisipoondoka na mtu
kitaondoka na bati. Wote wanashutumiwa
na matumizi mabaya ya Umma na Ufisadi,
wapelekwe mahakamani, sio kuwatumbua
kazini halafu wanaachwa Uraiani wakila
raha bila kuchukuliwa Sheria yoyote.
Tuiachie Mahakama Ihukumu au isafishe
Mtu.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top