Uju wa madaraka wa viongozi wa afrika rais wa chadi agombea mhula wa tano.
Rais wa Chad ambaye ni miongoni mwa marais
wa Afrika waliohudumu kwa mda mrefu
mamlakani anawania muhula wa tano wakati
ambapo wapiga kura watashiriki katika uchaguzi
mnamo tarehe 10 mwezi Aprili.
Idriss Deby amekuwa madarakani kwa takriban
miaka 26.
Rais Deby alitwaa madaraka kupitia mapinduzi ya
kijeshi mwaka wa 1990.
Tangu wakati huo hadi sasa ameendelea kuthibiti
taasisi muhimu za taifa na amekua mshirika wa
karibu na dola za magharibi katika vita dhidi ya
ugaidi.
Upinzani ulisusia uchaguzi mkuu wa mwaka 2011
na hivyo kumuwezesha kupata ushindi kwa
urahisi.
Mwaka huu japo kuna upinzani lakini Bw Deby
anatarajiwa kupata ushindi kutokana na
mgawanyiko miongoni mwa wapinzani wake.
Aidha mahakama ya kikatiba imemzuia mpinzani
wake mkuu kuwania pamoja na wagombea
wengine watano.
Vyombo vya usalama vimevunja maandamano ya
upinzani yanayomshinikiza Deby kuachia ngazi.
Kinyang'anyiro cha urais nchini Chad kimevutia
wagombea 13.
Idriss Deby anapeperusha bendera ya chama
tawala Patriotic Salvation Movement.
Wapinzani wake wawili ni mawaziri wake wa
zamani.
Ikiwa hakutakua na mshindi wa moja kwa moja
ambaye anafaa kushinda asilimia 50 ya kura,
basi itafanyika raundi ya pili ya kura ya urais kati
ya mshindi wa kwanza na wa pili.
Chad imekabiliwa na changamoto za kiusalama
tangu ijipatie uhuru wake kutoka kwa Ufaransa
mwaka 1958.
Katika siku za karibuni nchi hiyo imekabiliwa na
tishio la ugaidi kutokana na makundi yaliyo nchi
jirani ya Boko Haram ya Nigeria na kundi la Al
Qaeda tawi la Afrika Kaskazini linaloendesha
operesheni zake katika mataifa ya Sahel.chanzo bbc swahili.
0 comments :
Post a Comment