Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, April 10, 2016

Ombaomba wapigwa marufuku Dar.soma zaid

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda amepiga marufuku wananchi
wanaotoa Pesa kwa Omba omba kando ya
barabara kwa kuwa wanachangia uwapo
wa watu hao huku baadhi ya watu
wakiwatumia watoto hao kujipatia kipato
kinyume cha sheria.
Akizungumza jijini Dar Bw.Makonda
amesema kumekuwa na Ongezeko kubwa
la watoto katika barabara kadhaa za jiji la
Dar wakijihusisha na kuomba pesa huku
wanaowatuma wakiwa wamekaa pembeni
jambo ambalo ni kinyume na sheria lakini
pia linahatarisha Usalama wa watoto hao.
Aidha amesema mkakati uliokuwapo kwa
kushirikiana na Ustawi wa jamii,
TAMISEMI pamoja na manispaa
kuhakikisha kuwa watoto hao
wanakusanywa na kuwekwa katika vituo
maalum huku wanaohusika na kuwatumia
kufanya kazi hiyo wakichukuliwa hatua.
Chanzo: Channel ten
My take: Nchi yetu yenyewe omba omba
maarufu duniani, halafu unapiga
marufuku ombaomba??

0 comments :

Post a Comment

Back To Top