Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, May 14, 2016

Afisa wa ukaguzi Fifa amejiuzulu akipinga mabadiliko.soma zaid.

Afisa wa ukaguzi katika shirikisho la soka
duniani Fifa Domenico Scala,amejiuzulu akipinga
mabadiliko yanayofanyika katika shirikisho hilo.
Scala amekasirishwa na hatua ya Baraza jipya la
Fifa lenye uwezo wa kuajiri na kuwafuta kazi
wale wanaosimamia kamati zake ikiwemo ile ya
ukaguzi,maadili na fedha.
Baraza hilo lilichukua mahala pa kamati kuu ya
Fifa kufuatia madai ya ufisadi katika shirikisho
hilo.
''Kamati hizo sasa zitakuwa hazina uhuru
kutekeleza majukumu yake'',alisema Scala.
Ameongezea kuwa: Hatua hiyo inahujumu nguzo
ya uongozi mzuri wa Fifa na inaharibu ufanisi wa
mabadiliko yaliofanywa.
Scala alikuwa na jukumu muhimu katika
kusukuma mabadiliko kufuatia kashfa iliolazimu
kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa rais wa
shirikisho hilo Sepp Blatter na mwenzake wa
Uefa Michel Platini.chanzo bbc.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top