Hii hapa ni orodha ya mataifa fisadi Afrika mashariki ipi inaongoza? Soma zaid.
Baada ya waziri mkuu wa Uingereza David
Cameron kunaswa na kamera akiidunisha
Nigeria kuwa mafisadi wakuu kote duniani BBC
imeamua kuangazia kwa umakini ikiwa
matamshi hayo ni ya kweli.
Je Nigeria imeorodheshwa katika nafasi ipi katika
orodha ya mataifa fisadi kwa mujibu wa
shirikisho la kupambana dhidi ya ufisadi duniani
Transparency International ?
Ni vigumu kuelezea kwa kina ama hata kupiga
msasa ufisadi katika mataifa kwani kila
mwanauchumi anaelezea ufisadi akitumia mizani
tofauti na mwenziye.
Kwa sababu hiyo tutatumia orodha ya mwaka wa
2015 ya shirikisho la kupambana dhidi ya ufisadi,
Transparency International, ili kukupa taswira ya
mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki na jinsi
yanavyolinganishwa na mataifa mengine duniani
katika mizani ya ubadhirifu na wizi wa mali ya
uma.
Cha mno hata hivyo sharti tuweke bayana kuwa
Nigeria sio taifa fisadi zaidi duniani.
Nigeria imeorodheshwa katika nafasi ya 136
Nigeria kati ya mataifa 167.
Kenya kwa mfano inasemekana kuwa na ufisadi
mkubwa hata kuishinda Nigeria.
Katika kanda ya Afrika Mashariki , mali ya umma
inafujwa sana na viongozi wa serikali hali
ambayo inaiweka mataifa ya kanda katika nafasi
za mwisho mwisho kuashiria viwango vya juu vya
ufisadi.
Kati ya mataifa kumi Fisadi zaidi duniani Somalia
inaongoza ikifwatwa na Sudan ,Sudan Kusini,
Eritrea, Burundi, DRC, Uganda, Kenya Tanzania
Ethiopia na kisha Rwanda katika usanjari huo.
Somalia inaongoza kwa Ufisadi duniani katika
nafasi ya 167.
Viwango vya ufisadi vinanasibishwa na Korea
Kaskazini.
Nchi iliyojitenga kabisa na ufisadi kanda ya
Afrika Mashariki na kati ni Rwanda.
Taifa hilo linaloongozwa na rais Paul Kagame
linaorodheshwa katika nafasi ya 44 duniani.
Je unakumbuka rais Robert Mugabe
aliyewadunisha wakenya kwa kuwa wezi ?
Kulingana na orodha hii iliyotayarishwa na shirika
la TI Zimbabwe wanaorodheshwa katika nafasi
ya 150 duniani kwa ufisadi.
Wanagawana nafasi hiyo na Burundi.
Orodha ya mataifa 10 fisadi zaidi kanda ya Afrika
Mashariki na Duniani.
1. 167 Somalia / North Korea
2. 165 Sudan
3. 163 South Sudan/ Angola
4. 154 Eritrea/Yemen / Turkmenistan / Syria
5. 150 Burundi / Zimbabwe
6. 147 Democratic Republic of the Congo /
Chad / Myanmar /
7. 139 Kenya / Uganda
8. 117 Tanzania
9. 103 Ethiopia
10. 44 Rwanda.chanzo bbc swahil.
0 comments :
Post a Comment