Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, May 11, 2016

Mwanamke asimamishwa kazi kwa Kukataa kuvaa viatu vyenye visigino virefu.soma zaid.

Karani mmoja wa kupokea wageni mjini London
alilazimika kurudi nyumbani baada ya kukataa
kuvaa viatu vyenye visigino virefu,imebainika.
Mfanyikazi huyo wa kampuni ya Temp, Nicola
Thorp mwenye umri wa miaka 27 kutoka Hackney
aliwasili katika kampuni moja inayoshughulikia
maswala ya kifedha PwC kabla ya kuarifiwa
kwamba anahitajika kuvaa viatu vyenye visigino
vya nchi 2 hadi 4.
Alipokataa na kulalamika kwamba mbona
wenzake wa kiume hawakutakiwa kuvaa
hivyo,alitakiwa kurudi bila ya mshahara.
Kampuni ya Portico imesema kuwa iliweka sheria
hizo kwa wafanyikazi wanaokabidhiwa PwC lakini
imesema kuwa haitaondoa sheria hiyo.chanzo bbc swahil.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top