Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, May 11, 2016

Vivuko vitatu mkoani mwanza vimesimamishwa kutoa huduma ya usafiri.soma zaid

Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa
Mwanza, imesimamisha huduma za usafiri wa
vivuko vitatu vya kampuni ya Kamanga kuanzia
Jana hadi hapo wamiliki wake watakaporekebisha
baadhi ya dosari zilizobainishwa na wakaguzi
kutoka mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu
na majini (SUMATRA).
Agizo hilo la kuitaka kampuni ya kamanga Ferry
Ltd kusimamisha huduma za vivuko vyake
kuanzia jumatano Mei 11 mwaka huu limetolewa
na mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella
baada ya kutembelea katika kivuko cha
Kamanga, akiwa ameongozana na wajumbe wa
kamati ya ulinzi na usalama.
Afisa mfawidhi wa SUMATRA mkoa wa Mwanza
Kapteni Michael Rogers, Nusura naye atumbuliwe
na mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza kwa uzembe
wa kushindwa kusimamia maagizo yao, baada ya
cheti cha meli ya MV. Orion kumalizika muda
wake tangu Aprili 30 mwaka huu lakini kivuko
hicho kimeendelea kutoa huduma kama kawaida.
Afisa masoko wa kampuni ya kamanga Sadi
Abeid akaelekeza lawama kwa mamlaka ya
udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini
(SUMATRA), huku katibu mtendaji wa chama cha
kutetea abiria wanaotumia usafiri wa majini
kanda ya ziwa Marcel Rugambwa akiunga mkono
hatua ya serikali ya kuvifungia vivuko vya
kampuni hiyo.
Mhasibu wa kampuni ya Kamanga Ambrose
Kenzagi akajikuta mikononi mwa polisi kwa
madai ya kukaidi agizo la SUMATRA, kufuatia
wamiliki wa kampuni hiyo kuendelea kutoa
huduma ya usafiri wa abiria kwa kutumia kivuko
cha MV. Orion huku wakifahamu kuwa kina
makosa 13 yanayotakiwa kufanyiwa marekebish

0 comments :

Post a Comment

Back To Top