Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, May 11, 2016

Mgombea urais Donard Trump atakutana na wabunge wa republican alhamis.soma zaid.

Mitch McConnell, kiongozi wa walio wengi katika
baraza la seneti Marekani.
Warepublican katika baraza la seneti
wanaonekana kukubaliana na ukweli uliofikiriwa
ni miujiza kwamba mfanyabiashara bilionea wa
New York, Donald Trump ni mgombea rais
mtarajiwa katika chama chao.
Trump alishinda uteuzi kwa njia ya kizamani
inayotumika kwa kupata kura nyingi kuliko
mgombea mwingine yeyote alisema kiongozi wa
walio wengi katika seneti, Mitch McConnell
Jumanne baada ya miezi kadhaa ya kukataa kuto
maoni yake juu ya mchakato wa kinyang’anyiro
cha urais.
Alisema “tunaheshimu sauti za wapiga kura wa
Republican katika uchaguzi wa awali kote
nchini”. Trump anatarajiwa kukutana na wabunge
wa Republican katika mabaraza yote mawili siku
ya Alhamis, atakutana ana kwa ana na baadhi
yao ambao wameelezea kutomuunga mkono
katika harakati zake za kuwania uteuzi,
ikimjumuisha spika wa bunge Paul Ryan ambaye
amekataa kumuidhinisha Trump.chanzo voa swahil.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top