Mvua kubwa iliyonyesha ethiopia imesababisha maafa ya watu 50.soms zaid.
Takriban watu 50 wamefariki kufautia
mafuriko na maporomoko ya ardhi
yaliosababishwa na mvua kubwa katika
baadhi ya maeneo Ethiopia.
Taifa hilo la upembe wa Afrika
linakabiliwana ukame mbaya kuwahi
kushuhudiwa katika miaka 50 huku watu
zaidi ya milioni 10 wakiwa wanahitaji
msaada wa dharura wa kibinaadamu.
Ukame huo umezidhishwa kuwa mbaya
kutokana mvua ya El Nino inayoaathiri
baadhi ya mataifa Afrika mashariki na
kusini.
Maafisa wa serikali katika wilaya iliopo
kusini mwa Ethiopia Wolaita wamekiambia
kituo cha televisheni ya serikali kuwa
watu 41 waliuawa Jumatatu katika
maporomoko ya ardhi yaliotokana na
mvua kubwa inayoendelea kunyesha
nchini.
Wengine 9 walifariki kusini mashariki
mwa eneo la Bol ambako mamia ya
mifugo pia ilizama.
Maelfu ya watu pia wamepoteza makazi
yao, walisema maafisa.
Mafuriko yametatiza jitihada za
kuwaisaidia watu wanaohitaji usaidizi
baada ya barabara nyingi na vivukio
kuharibika kabisa.
Serikali na mashirika ya misaada
yameanzisha ombi la msaada wa thamani
ya dola bilioni 1.4 kuwasiaidia mamilioni
ya watu wanaohitaji kwa dharura chakula.
Chanzo: BBC
0 comments :
Post a Comment