Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, May 18, 2016

Msimamo wa kambi ya upinzani bungeni ni kumtaja hadharani mtu yeyote ayebainika kuhujumu ujuchumi taifa.soma zaid.

Wabunge wameendelea kuijadili bajeti ya wizara
ya ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano huku kiongozi
mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni
Mhe.Freeman Mbowe akiliambia bunge hilo kuwa
msimamo wa kambi hiyo ni kumtaja hadharani na
kumshutumu mtu yeyote ambaye alishiriki ama
anashiriki katika kulihujumu taifa bila kujali kama
yupo Serikalini ama kambi ya upinzani.
Kiongozi huyo mkuu wa kambi hiyo ya upinzani
amesema hayo kufuatia wabunge kupitia chama
cha mapinduzi kumshutumu aliyekuwa Waziri
mkuu wakati uuzaji wa nyumba hizo za Serikali
Mhe.Edward Lowasa ambaye sasa ni mjumbe wa
kamati kuu ya chadema kuwa naye alishiriki
katika uuzaji wa nyumba hizo kwani Rais wa
sasa Dr.John Magufuli alikuwa waziri wa ujenzi
na Mhe.Lowasa alikuwa bosi wa Dr.Magufuli
kama Waziri Mkuu.chanzo itv

0 comments :

Post a Comment

Back To Top