Kizza Besigye amekutwa na kosa la uhaini mahakamani nchini uganda.soma zaid.
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza
Besigye amefikishwa mahakamani mjini
Kampala na kushtakiwa kwa kosa la uhaini.
Dkt Besigye alifikishwa katika majengo ya
mahakama ya Nakawa mapema kabla ya saa
tatu, muda wa kawaida wa kufunguliwa kwa
mahakama, na akasomewa mashtaka.
Alijiwakilisha mwenyewe kortini na amesema
hataki kuhusisha mawakili katika kesi hiyo.
Hakimu ameamuru awekwe rumande hadi tarehe
1 Juni.
Dkt Besigye ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa
Rais Yoweri Museveni kwenye uchaguzi mkuu
uliofanyika Februari nchini humo.
Leo imekuwa mara ya pili kufikishwa
mahakamani akikabiliwa na tuhuma hizo za
uhaini kwani awali alifikishwa mahakani kwa
mara ya kwanza siku ya Ijumaa iliyopita katika
mji wa Moroto, baada yake kudaiwa kujiapisha
kuwa rais siku moja kabla ya Rais Museveni,
aliyetangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo
kuapishwa..
Besigye alishikiliwa na polisi kwa muda wa siku
mbili ambapo alifikishwa mahakamani huku
shughuli za mahakama zikiwa zimekwisha.
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wafuasi
wake ambao wamekuwa wakisema hakuruhusiwa
kuwasiliana na wanasheria wake.chanzo bbc.
0 comments :
Post a Comment