Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, May 18, 2016

John Tery atabakia tena katika klabu ya chelsea baada ya kusain mwaka mmoja.soma zaid.


Beki wa Chelsea John Terry ametia saini
kandarasi mpya ya mwaka mmoja na kibu hiyo
ya Uingereza.
Katika hotuba iliojaa hisia baada ya mechi ya
mwisho dhidi ya Leiceter siku ya
Jumapili,mchezaji huyo mwenye umri wa miaka
35 ambaye kandarasi yake ilikuwa imekamilika
alisema kuwa angependa kusalia katika klabu
hiyo.
''Kila mtu anajua mimi ni shabiki wa Chelsea
'',alisema beki huyo wa Uingereza.
''Nasubiri msimu ujao tukiwa na mkufunzi mpya
na natumai tutafanikiwa''.
Terry ameichezea Chelsea mara 703 katika kikosi
cha kwanza cha timu hiyo baada ya kuanza
kucheza soka katika kilabu hiyo mwaka 1998.
Mwenyekiti wa klabu hiyo Bruce Buck alisema
kuwa: tunafurahi kwamba John atahudumia
mwaka mwengine akiwa katika klabu hii.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top