Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, May 18, 2016

Jeshi la marekani linaangalia uwezekano wa kufunga vituo 11 barani Afrika.soma zaid.

Jeshi la Marekani linaangalia uwezekano wa
kufungua maeneo 11 ya kituo cha pili barani
Afrika kwa mujibu wa msemaji wa AFRICOM.
Kanali Mark Cheadle, alizungumza na sauti ya
Amerika-akizungumz  mjini Brussels hapo Jumanne
lakini hakuelezea maeneo yapi jeshi linafikiria
uwezekano wa kuwa na kituo cha pili, zaidi ya
kuelezea kwamba Nigeria sio mojawapo.
Marekani kwa sasa ina kituo kimoja cha kijeshi
katika taifa la Djibouti huko Afrika ya mashariki.
Vikosi vya Marekani pia vipo nchi kavu nchini
Somalia ili kusaidia mapigano ya kieneo dhidi ya
kundi la wanamgambo wa al-Shabaab na nchini
Cameroon ili kusaidia juhudi za mataifa mbali
mbali kupambana dhidi ya kundi la Boko Haram
lenye makao yake nchini Nigeria.
Kamanda wa AFRICOM, Jeneral David Rodriguez
Kamanda wa AFRICOM, Jenerali David Rodriguez
aliwaambia waandishi wa habari mjini Brussels
kwamba jeshi la Marekani liliwapa mafunzo
wanajeshi wa kikosi cha ki-intelijensia cha
Nigeria pamoja na wanajeshi watatu wa
mapigano huko Nigeria akiwemo mmoja ambaye
ndio kwanza amehitimu.
Huenda ukapenda pia.chanzo voa swahil

0 comments :

Post a Comment

Back To Top