Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, May 19, 2016

Serikali imetangaza rasimi bendera ya jumuiya ya Afrika mashariki.

Serikali imetangaza rasmi alama za
Jumuiya ya Afrika Mashariki
zitakazotumika kwenye Ofisi zote za
Serikali na katika shughuli zote rasmi za
kiserikali.
Aidha Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda
na Kimataifa Mindi Kasiga amezitaja alama
hizo kuwa ni bendera ya Taifa, bendera ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki, wimbo wa
Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na wimbo
wa Taifa.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki inaratibu upatikanaji
wa sampuli ya alama hizo kwa gharama
za taasisi, wizara au Ofisi husika.
Pia mkuu huyo wa kitengo cha
mawasiliano ndugu Kasiga amesema
kuanzia sasa bendera ya Jumuiya hiyo
itapepea sambamba na Bendera ya Taifa
kwenye Ofisi zote za Serikali huku wimbo
wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki
ukiimbwa sambamba na wimbo wa Taifa
katika shughuli rasmi za serikali kuanzia
ngazi za Halmashauri hadi Taifa, hii ikiwa
ni hatua ya utekelezaji wa Mkataba wa
uanzishwaji wa jumuiya hiyo kifungu cha
7(a).
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa
wizara ya mambo ya nje amenukuliwa
akisema “Mkataba huu unasisitiza jumuiya
hii kuwa jumuiya ya watu, hivyo
watanzania watahusishwa katika hatua
zote za mtangamano huo, pamoja na
kushirikishwa kikamilifu katika hatua
mbalimbali za jumuiya ili kujua
madhumuni ya kunufaika na fursa
mbalimbali zitakazaopatikana ndani ya
Jumuiya hiyo”, Mwisho wa kunukuu.
Matumizi ya alama hizi ni njia mojawapo
ya kujenga uzalendo na kumfanya
Mwananchi ajisikie kuwa sehemu ya
ushirikiano huu.
Vilevile, taasisi binafsi zinaweza kutumia
alama hizi, huku shule na vyuo
vikisisitizwa kutumia alama hizi kama
sehemu ya kuelimisha na kuhamasisha
vijana kuhusu Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top