Kundi la Al-shabaab kimefanya mashambulizi katika kituo kimoja cha jeshi la kenya(KDF).soma zaid.
Kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab lenye
makao yake huko Somalia.
Shirikisha
Wanamgambo wa kundi la al-Shabaab wamedai
kushambulia kituo kimoja cha jeshi la Kenya
kilichopo eneo la kusini-magharibi mwa Gedo
nchini Somalia siku ya Jumatano.
Kwa mujibu wa ripoti ya mtandao wa habari wa
Shabelle kundi la al-Shabaab lilisababisha hasara
kubwa dhidi ya wanajeshi wa KDF katika
shambulizi hilo katika kijiji cha Fahahdhum huko
Gedo.
Katika shambulizi jingine wanamgambo
wamefanya shambulizi la papo hapo na kukimbia
dhidi ya vikosi vya Kenya vilivyo kwenye kituo
cha ukaguzi katika mji wa Hosingow uliopo
kwenye mkoa wa Lower Jubba.
Mji wa Hosingow hivi sasa unadhibitiwa na jeshi
la Kenya na vikosi vya Jubbaland.
Wanamgambo wa al-Shabaab walisema waliuteka
nyara kwa muda mji huo baada ya kuwazidi
nguvu wanajeshi wa KDF na Jubbaland wakati
wa shambulizi. Lakini hakukuwa na uthibitisho
huru kuhusiana na taarifa hizo.VOA swahil.
0 comments :
Post a Comment