February 20, 2025
Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, May 19, 2016

Mchungaji ahukumiwa kwenda jela kwa kutapeli.soma zaid.

Kapenye amekuhumiwa kifungo hicho leo katika
mahakama ya wilaya ya Ilala ambapo mbali na
kifungo hicho, mchungaji huyo ametakiwa kulipa
fidia ya Sh13.7m alizotapeli.
Dar Es Salaaam. Mchungaji wa Kanisa la Hopran
Mission lililopo Tabata Kinyerezi, Jimmy Kapenye
(42) amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja
jela au kulipa faini ya Sh2m baada ya kupatikana
na hatia ya kutapeli Sh13.7m, mali ya askofu wa
kanisa hilo.
Kapenye amekuhumiwa kifungo hicho leo katika
mahakama ya wilaya ya Ilala ambapo mbali na
kifungo hicho, mchungaji huyo ametakiwa kulipa
fidia ya Sh13.7m alizotapeli.
Mchungaji huyo anadaiwa kupewa mahindi na
alizeti yenye thamani ya Sh13.7m na askofu wa
kanisa hilo, Charles Nicholas kwa ajili ya kuuza
na fedha itakayopatikana itumike kulipa mkopo
wa trekta ambalo waumini walikopeshwa na
Suma JKT. Hakufanya hivyo.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu wa Wilaya ya
Ilala, Maua Hamduni amesema mahakama yake
imeridhishwa na ushahidi wa mashahidi watatu
wa upande wa mashtaka waliotoa dhidi ya
mshtakiwa huyo.
“Kutokana na ushahidi ulitolewa na mashahidi wa
upande wa mashtaka, mahakama inakuhukumu
kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya
Sh2m na kulipa fidia ya Sh 13.7milioni ili liwe
fundisho kwa watu wote wenye tabia kama hizi
ambao ni viongozi wa dini,” alisema Hakimu
Hamduni.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, mahakama
ilitoa nafasi kwa mshtakiwa kujitetea kwanini
asipewe adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka
10 jela na mshtakiwa huyo alijitetea kuwa
apunguziwe adhabu kwa kuwa ana maradhi ya
tezi dume na ana familia inayomtegemea.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top