Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, May 19, 2016

Morogoro,kigoma,bonde la Rubada huko mto Rufiji kujengwa viwanda vya sukari.soma zaid.

Majaliwa: Rais hakukosea kuzuia sukari
kuingia nchini kiholela
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema
kauli ya Rais John Pombe magufuli ya
kuzuia kuingizwa kwa sukari kiholela
nchini ilikuwa ni katika kulinda viwanda
vya ndani.
Aidha Majaliwa amesema kuingia kwa
sukari Tani 70,000 toka nje ya nchi
hakutaathiri uzalishaji wa viwanda
unaotarajiwa kuanza mapema mwezi julai.
Akijibu swali la kiongozi wa kambi ya
upinzani bungeni na mbunge wa jimbo la
Hai,Freeman Mbowe, Majaliwa amesema
uhaba wa sukari ni tani 100,000 na
uwezo wa viwanda kuzalisha ni tani
320,000 huku mahitaji ya sukari kwa
mwaka mzima ni tani 420,000.
Serikali inaendelea na mazungumzo na
wawekezaji wanaokusudia kuwekeza
katika viwanda vya sukari ili kuongeza
uwezo wa uzalishaji kwa ajili ya
kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo
nchiniKauli hiyo imetolewa leo mjini
Dodoma na Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa wakati akijibu maswali ya papo
kwa papo ya kila Alhamis.
Alisema kuwa lengo la mazungumzo ya
kutaka viwanda viweze kuongeza
uzalishaji wa sukari ili uweze kufikia tani
420,000 katika kipindi miaka minne ijayo
na hivyo kupunguza uagizaji wa sukari
kutoka nje ya nchi. Mhe. Majaliwa
alisema kuwa maeneo ambayo
yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa
viwanda vipya ya Sukari ni pamoja na
Kigoma, Morogoro na Bonde la Rubada
lilipo katika mto Rufiji.
Kuhusu kutojengwa kiwanda cha Sukari
katika eneo la Bagamoyo, Waziri Mkuu
alisema kuwa Serikali ilikataa kuruhusu
ujenzi wa kiwanda cha Sukari katika eneo
hilo baada ya Kamati ya Bunge kushauri
kuwa kisijengwe kwa sababu
kingehatarisha uhai wa wanyama waliomo
katika Mbuga ya Saadan kwa kuwa
kingetumia maji mengi kutoka Mto Wami.
Mhe. Majaliwa alisema kuwa hali hiyo
ingesababisha upungufu wa maji ambayo
ni tegemeo kwa wanyama wa Mbuga ya
Saadan yambao ni muhimu kwa sekta ya
utalii nchini.Kwa upande wa upungufu wa
sukari nchini, Waziri Mkuu alisema kuwa
Serikali imeagiza tani 70,000 kutoka nje
ya nchi.
Alisema kuwa mahitaji ya sukari ni tani
420,000 lakini zilizopo ni tani 320,000 na
kuwepo kwa upungufu wa tani
100,000.Mhe. Majaliwa alisema kuwa
Bodi ya Sukari nchini ili kukabiliana
upungufu huo imeweka utaratibu wa
uagizaji huo ili kuhakikisha Waagizaji wa
Sukari nje wasije wakaingiza sukari nyingi
kinyume cha inayohitajika na hivyo
kuathiri viwanda vya hapa nchini.
Aliongeza kuwa Bodi hiyo kwa
kushirikiana Mamlaka ya Mapato nchini
(TRA ) itasimamia kuhakikisha kuwa
sukari inayoingiza nchini ndio
inayohitajika. Kuhusu bei elekezi ya
sukari, Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali
inaweka kiwango ili kumlinda mwananchi
wa kawaida.
Kwa upande wa upungufu wa sukari
nchini, Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali
imeagiza tani 70,000 kutoka nje ya
nchi.Alisema kuwa mahitaji ya sukari ni
tani 420,000 lakini zilizopo ni tani
320,000 na kuwepo kwa upungufu wa
tani 100,000.
Mhe. Majaliwa alisema kuwa Bodi ya
Sukari nchini ili kukabiliana upungufu huo
imeweka utaratibu wa uagizaji huo ili
kuhakikisha Waagizaji wa Sukari nje
wasije wakaingiza sukari nyingi kinyume
cha inayohitajika na hivyo kuathiri
viwanda vya hapa nchini.Aliongeza kuwa
Bodi hiyo kwa kushirikiana Mamlaka ya
Mapato nchini (TRA ) itasimamia
kuhakikisha kuwa sukari inayoingiza
nchini ndio inayohitajika.
Kuhusu bei elekezi ya sukari , Waziri
Mkuu alisema kuwa Serikali inaweka
kiwango ili kumlinda mwananchi wa
kawaida.Alisema kuwa bei hiyo
zinazingatia gharama zote ikiwemo
usafirishaji kuto ka zinapoagizwa na
kumfikia mlaji.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top