Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, May 31, 2016

Mwalimu apandishwa mahakani kwa kugushi vyeti.soma zaid.


Dar es Salaam. Mwalimu wa Shule ya Msingi
Kisutu, Marth Komanya amepandishwa kizimbani
katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu
mashtaka manne yanayomkabili likiwamo la
kugushi cheti cha ualimu.
Mshtakiwa amefikishwa mahakamani hapo leo na
kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi
Catherine Kiyoja.
Wakili wa Serikali, Grace Mwanga amedai
mahakamani hapo kuwa siku zisizojulikana
mshtakiwa alighushi cheti chenye namba S.
375\55 ambacho kilionyesha amemaliza elimu ya
sekondari wakati akijua kuwa siyo kweli.
Shtaka la pili, mwalimu huyo amedaiwa
kuwasilisha nyaraka katika Manispaa ya Ilala
ambazo zilikuwa zinaonyesha amemaliza elimu
ya sekondari wakati akijua siyo kweli.
Mwanga amedai katika shtaka la tatu na nne
kuwa mshtakiwa amegushi cheti cha ualimu
chenye namba 71844 kikionyesha alipata daraja
la 3A na kuwasilisha katika Manispaa ya Ilala,
wakati akijua kuwa ni uongo.
Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka
yanayomkabili alikana kutenda makosa hayo.
Hakimu Kiyoja ameahirisha kesi hiyo hadi Juni
13, mwaka huu itakapotajwa tena.
Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya
kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili
ambao ni wafanyakazi kutoka taasisi
inayotambulika kisheria waliosaini bondi ya Sh2
milioni kila mmoja.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top