February 19, 2025
Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, May 12, 2016

Serikal kukagua dawa zinazoingia katika bandari ya Dar es salaam.soma zaid.

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, imetangaza mkakati wa
ukaguzi wa dawa zinapoingia katika Bandari ya
Dar es Salaam ikiwa ni mkakati wa kuzuia
upotevu.
Imesema imeandaa mpango unaojulikana kama
‘Pilferage Tool’ ambao utatumika kufanya
ukaguzi wa upotevu wa dawa unaosadikia
kutokea kuanzia mzigo unapoingia bandarini
mpaka kumfikia mgonjwa.
Mkakati huo ulitangazwa jana bungeni mjini hapa
na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alipowasilisha
bajeti ya wizara yake ya Sh bilioni 277.6.
Alisema mfumo huo utasaidia upatikaji wa dawa
kwa hospitali zote nchini.
Waziri alisema pia kuwa Serikali imefanya
mapitio ya kina ya mfumo wa ununuzi na
utunzaji wa dawa katika Bohari Kuu ya Dawa
(MSD).
“Ili kuepuka kulipa kodi na tozo zilizo juu
kutokana na misaada inayoletwa nchini bila kuwa
na utaratibu maalumu wa kupokea misaada hiyo.
“Wizara itatoa mafunzo ya kusambaza na
kusimamia utekelezaji wa mwongozo wa ufanisi
wa kazi kupitia mfumo wa 5S Kaizen TQM
kuimarisha usimamizi wa takwimu za dawa,”
alisema Ummy.
Alisema wizara imeendelea kuboresha huduma ya
afya ya uzazi na motto na katika mwaka 2015/16
iliwajengea uwezo watoa huduma jinsi ya
kumhudumia mtoto aliyezaliwa na upungufu wa
uzito.
Licha ya hali hiyo suala la vifo vinavyotokana na
uzazi bado ni changamoto ambako kutokana na
taarifa za Umoja wa Mataifa (UN), Tanzania
imepunguza vifo hivyo kutoka 454 mwaka 2010
hadi 398 mwaka 2015.
“Ili kuhakikisha vifo hivi vinaendelea kupungua
kwa kasi zaidi wizara imehakikisha watoa
huduma wa afya 2,087 wamejengewa uwezo kwa
kuwapatia mafunzo ya huduma muhimu wakati
wa ujauzito, stadi za kuokoa maisha kwa
matatizo ya dharura yatokanayo na mtoto
mchanga na baada ya kujifungua,” alisema.
Akizungumzia huduma za chanjo, alisema wizara
itaendelea kutoa miongozo ya huduma za chanjo
kulingana na miongozo.
“Pia Wizara imeendelea na juhudi za kudhibiti
UKIMWI kwa kutoa ushauri nasaha na kupima na
kuanzia Januari hadi Desemba mwaka jana,
wateja wapya 3,474,780 walipata ushauri nasaha
na kupima VVU.
“Na idadi hii inajumulisha pia waliopata huduma
kupitia mpango wa kuzuia maambukizi ya VVU
kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto PMTCT,”
alisema.
Maoni ya upinzani
Akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni, Msemaji wa Mkuu wa wizara hiyo, Dk.
Godwin Mollel, alisema suala la upungufu wa
madawa unaweza kuongezeka kwani Serikali
imetenga Sh bilioni 65.1 kwa ajili ya ununuzi wa
dawa.
Alisema kiasi hicho kinatosha mahitaji ya nchi
kwa mwezi mmoja na nusu tu kwa kukadiria
kuwa Tanzania ina watu takribani milioni 49.8
wanaohitaji matibabu, kiasi kilichotengwa
kinatosha kutibu watu milioni 5.6 kwa mwaka.
“Je, watu wengine milioni 44 wanaobaki
watatibiwa na nini na wapi? Mheshimiwa Spika:
Kambi Rasmi ya Upinzani inaishauri Serikali
iongeze bajeti ya madawa kutoka asilimia 11
(bilioni 65.1) mpaka angalau asilimia 50 ya
mahitaji (bilioni 295.9).

0 comments :

Post a Comment

Back To Top