Mwanamziki Rihanna ameguswa na suala la Elimu na huu ni mchango wake katika elimu.soma zaid.
Nyota wa muziki Rihanna amejitolea kufadhili
elimu ya wanafunzi kupitia wakfu wake.
Hatua hiyo inaamanisha kwamba watu kutoka
jamii zisizojiweza watapata msaada wa kulipa
ada ya shule.
Wakfu huo wa Clara Lionel umekuwa ukifanya
kazi tangu 2012 ambapo hutoa ruzuku kwa shule
huko Barbados mbali na kuwasaidia wagonjwa
wa saratani.
Bibiye Rihana alifariki kutokana na ugonjwa wa
saratani mwaka huo huo na hivyobasi kumfanya
yeye kuanza kusaidia sekta ya matibabu.
Kwa sasa shirika hilo limepanuka na kutoa
ufadhili wa elimu hadi kufikia dola 50,000 kwa
wanafunzi waliopo
Barbados,Brazil,Cuba,Haiti,Guyana,Jamaica na
Marekani.
''Sidhani kwamba ni haki kwa watoto kubeba
mzigo wa kifedha katika miaka walio
nayo'',alisema Rihanna.chanzo bbc.
0 comments :
Post a Comment