Serikal yasitisha ajira za majeshi.soma zaid.
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesitisha
kwa muda ajira zote kwenye vyombo vya ulinzi
na usalama vilivyomo ndani ya wizara hiyo,
ikiwemo Jeshi la Polisi ili kupitia upya utaratibu
wa kutoa ajira na kuondoa uwezekano wa watu
wasio na sifa kujipenyeza.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Hamad Masauni alisema hayo jana bungeni
wakati akijibu swali la Mbunge wa Moshi Vijijini,
Anthony Komu (Chadema), aliyetaka kufahamu ni
kwa nini Serikali inasitisha ajira katika Jeshi la
Polisi, wakati bado nchi inakabiliwa na uhaba wa
askari ndani ya jeshi hilo wakiwemo askari wa
kike.
“Tumesitisha kutoa ajira ndani ya Wizara ya
Mambo ya Ndani ili kuondoa uwezekano wa watu
wasio na sifa kujipenyeza na kupata ajira ndani
ya vyombo vilivyo chini ya wizara hiyo,”
alisisitiza.
Miongoni mwa vyombo hivyo vilivyopo chini ya
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mbali na
Jeshi la Polisi ni Jeshi la Magereza, Jeshi la
Zimamoto na Uhamiaji. Mbali na Komu, Mbunge
mwingine ambaye ni wa Viti Maalumu, Hawa
Mwaifunga (Chadema), alitaka kufahamu Serikali
inachukua hatua gani kuhakikisha askari wasio na
sifa wanachukuliwa hatua, ambapo pia alitaka
kufahamu utaratibu wa uhakiki vyeti vya askari
wasio na sifa ndani ya Jeshi la Polisi umefikia
wapi.
Akizungumzia Jeshi la Polisi, Masauni alisema
Jeshi la Polisi limo kwenye utaratibu wa
kuwachukulia hatua za kisheria askari wachache,
wanaochafua taswira na kazi nzuri inayofanywa
na Polisi kwa kukiuka sheria, kanuni na taratibu
kwa kujihusisha na vitendo vinavyokinzana na
maadili.
Kuhusu uhakiki wa vyeti, waziri huyo alielezea
kuwa, uhakiki huo unahusu askari wasio na sifa
ndani ya Jeshi la Polisi unaendelea na mpaka
sasa, askari 19 wamechukuliwa hatua za kisheria
baada ya kugundulika kuwa walipata ajira kwa
njia zisizokubalika.
Kuhusu uhaba wa askari wa kike, Waziri huyo
alikiri kuwa kuna uhaba wa askari wa kike katika
Jeshi la Polisi na kutoa mwito kwa wanawake
wahamasike zaidi kujiunga na vyombo vya
usalama.
Mwaka jana Idara ya Uhamiaji iliyokuwa chini ya
Wizara hiyo, ililazimika kufuta ajira mpya 200 za
makonstebo na makoplo, baada ya kubaini
upatikanaji wa ajira hizo, ulifanyika kwa
upendeleo.chanzo gazet habari leo.
0 comments :
Post a Comment