Breaking News
Loading...

Advert

Friday, May 13, 2016

TFDA imetoa taarifa ya utekelezaji wa shehena za vyakula na dawa 2015/2016

Mamlaka ya chakula na dawa TFDA imetoa
taarifa ya uteketezaji wa shehena ya vyakula,
dawa, vifaa tiba na vipodozi vilivyopigwa
marufuku nchini au kumaliza muda wa matumizi
kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ambapo
thamani yake ni zaidi ya shilingi milioni 900 huku
maeneo yanayoongoza kwa kuingiza bidhaa hizo
ni kwenye mipaka hasa mikoa ya magharibi na
kanda ya ziwa kupitia mwambao wa ziwa
Victoria na Tanganyika.
Hii ni shehena ya dawa, vyakula, vifaa tiba na
vipodozi ambavyo havifai kwa matumizi ya
binadamu zaidi ya tani nne vilivyokamatwa
Dodoma na kuteketezwa kwenye dampo hili
ambapo mkurugenzi mkuu wa TFDA Hiiti Silo
anasema kwa mwaka wa fedha 2015/16 bidhaa
hizo zenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni
900 vimekamatwa huku akitoa wito kwa
wananchi kuepuka matumizi yake kwani yana
madhara makubwa kwenye afya.
Sifa Chalugenzi ni mkaguzi wa chakula na dawa
na vipodozi kutoka TFDA kanda ya kati anasema
kuongezeka kwa matumizi ya vyakula na vipodozi
vilivyopigwa marufuku nchini kunachagia
kuendelea kuwepo kwa maradhi yakiwemo ya
saratani hasa ya ngozi huku waathirika wakubwa
wakiwa ni wanawake.
Katika zoezi la uteketezaji wa bidhaa hizo
ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu afisa
afya wa manispaa ya Dodoma Alec Balankena
anatoa wito kwa wakazi wa mji huo kujenga
utamaduni wa kusoma maelezo yaliyopo kwenye
bidhaa kabla ya kununua ili kujua kama zinafaa
kwa matumizi au la.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top