TEWUTA yalia na makampuni ya simu.soma zaid.
Akiongea leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa
Taifa wa TEWUTA, Bw. Pius Makuke, amesema
wamefikia uamuzi huo kwa sasa baada ya kuona
kuwa Serikali kupitia mamlaka zake zinapuuzia
malalamiko ya wafanyakazi katika kampuni za
simu ambayo yameendelea kutolewa.
Bw. Makuke ameogeza kuwa endapo hata kilio
chao kisiposikilizwa kupitia migomo ambayo
watatangaza basi watafanya taratibu nyingine za
kisheria ikiwemo kwenda mahakamani ingawa
kwa sasa wametoa siku hizo 30 ili kusikilizwa
maombi yao.
Mwenyekiti huyowa TEWUTA amebainisha kati ya
mambo ambayo wanayapigania ikiwa ni pamoja
na mikata ya kudumu katika makampuni ya
simu, uwasilishwaji mafao katika mifuko ya
hifadhi ya jamii pamoja na ubaguzi kwa
wafanyakazi wazawa.
0 comments :
Post a Comment