Breaking News
Loading...

Advert

Monday, June 6, 2016

Hakuna mwenye ubavu wa kukifuta chama cha CUF zanzibar.soma zaid.

Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma
wa CUF, Salim Bimani
Mwinyi Sadallah – Nipashe
Jumatatu, 6 Juni 2016
MGOGORO wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar,
umechukua sura mpya baada ya Chama cha
Wananchi (CUF), kusema hakuna Mamlaka
Zanzibar yenye ubavu wa kukifutia usajili
kutokana na msimamo wake wa kutomtambua Dk
Ali Mohamed Shein na serikali yake.
Tamko hilo lilitolewa mjini Zanzibar jana na
Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma
wa chama hicho, Salim Bimani kufuatia hoja
binafsi iliyopitishwa na Wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar (BLW) wakitaka CUF
kifutiwe usajili kama kikithibitika kufanya siasa
za ubaguzi kinyume cha sheria namba tano ya
vyama vya siasa ya mwaka 1995.
Alisema CUF kitaendelea kubakia na msimamo
wake wa kutoitambua Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar (SMZ) pamoja na Baraza la Wawakilishi
mpaka Dk Shein aondoke madarakani.
“Serikali ya Zanzibar na Baraza la Wawakilishi,
hawana ubavu wa kuifuta CUF kwa mujibu wa
Sheria ya Vyama vya Siasa Namba tano ya
mwaka 1995,” alisisitiza Bimani.
Alisema vyama vya siasa vinasimamiwa na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
nchini.
Alisema hoja binafsi ya kutaka CUF kuchuguzwa
na kufutiwa usajili, haina msingi wa nguvu ya
hoja na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
wanatafuta kukimbia chimbuko la mgogoro wa
uchaguzi mkuu Zanzibar.
Bimani alisema kama kufutiwa usajili, CCM ndiyo
iliyotakiwa kufutiwa kutokana na kuwapo kwa
malalamiko ya watu kunyimwa ajira na
kubaguliwa kupewa vitambulisho vya Mzanzibari
mkaazi kwa sababu za kisiasa.
Alisema mgogoro wa uchaguzi wa Zanzibar,
umetokana na CCM kutokuwa tayari kukubali
mabadiliko ya kiutawala kupitia njia ya
kidemokrasia tangu kuanzishwa kwa mfumo wa
vyama vingi vya siasa mwaka 1992.
Aidha, alisema migomo ndiyo silaha ya wanyonge
katika kutafuta haki na wapo wanasiasa
mbalimbali duniani walitumia migomo na kufikia
malengo yao.
Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu wa zamani wa
Zanzibar, Hamid Mbwezereni, alisema hakuna
njia ya kumuondoa madarakani Rais wa Zanzibar,
Dk Shein mpaka Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Alisema kampeni zinazofanywa na CUF za
kuwataka watu wabaguane au kususia kulipa
kodi, havina manufaa kwa Zanzibar na wananchi
wake.
“Nafasi pekee ya kumuondoa madarakani Dk
Shein ilikuwa uchaguzi mkuu wa marudio lakini,
CUF walisusia na hakuna njia nyingine mpaka
uchaguzi mwengine baada ya miaka mitano
mwaka 2020,” alisisitiza Mbwezereni.
Aliongeza kuwa wakati umefika kwa wanasiasa
Zanzibar, kuheshimu utawala wa sheria na kama
wana malalamiko ya msingi, walitakiwa kutumia
mahakama kutafuta haki, lakini wameshindwa
tangu kufanyika uchaguzi wa kwanza na
wamarudio Zanzi

0 comments :

Post a Comment

Back To Top