Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, June 30, 2016

Jambazi auwawa katika majibizàno ya risasi na polisi mkoani kigoma.soma zaid.

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limekabiliana kwa risasi na kundi la majambazi katika msitu wa Maghorofani katika barabara ya Kigoma-Mpanda ,na kufanikiwa kumuua mtu mmoja na kukamata bunduki moja ya kivita aina ya SMG na risasi 74 zilizokuwa zitumike kufanya utekaji wa magari katika barabara hiyo. Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi Ferdinand Mtui amesema awali polisi walimkamata mtuhumiwa Hamis Kabeteye mkazi wa kijiji cha Kitahana wilayani Kibondo, na kufanikiwa kupata risasi 51 katika kijiji cha Kalenge wilayani Uvinza,ambapo baada ya mahojiano aliwapeleka eneo la tukio ambako walikabiliana na wenzake waliokuwa wanajiandaa kuteka magari ambapo walifanikiwa kukimbia huku mtuhumiwa mmoja akiuawa,na polisi kufanikiwa kupata risasi zaidi . Katika hatua nyingine polisi wamekamata zaidi ya pikipiki mia nne na bajaji thelathini kutokana na makosa ya usalama barabarani ikiwa ni pamoja na madereva wake kutokuwa na leseni na kutozingatia sheria za usalama barabarani.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top