Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, June 25, 2016

Mafisadi na wahujumu uchumi sasa kukiona cha moto na hii ndio sheria. Soma zaid.

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
jana lilipitisha kwa kauli moja Sheria ya
Marekebisho Mbalimnbali, ambayo pamoja na
mambo mengine, yamempa Jaji Mkuu mamlaka
ya kuanzisha Divisheni ya Rushwa na Uhujumu
Uchumi ya Mahakama Kuu.
Kwa mujibu wa muswada huo uliowasilishwa na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju,
adhabu kwa watakaokutwa na hatia
zimeongezwa, huku mahakama hiyo ikiwekewa
mazingira wezeshi ili iendeshe kesi hizo kwa
haraka.
Mazingira wezeshi Muswada huo wa sheria
ambao kwa sasa utakuwa ukisubiri Rais ausaini
ili iwe sheria kamili, umekusudia kuanzisha
divisheni hiyo ya mahakama, ambayo itakuwa na
majaji wake na watumishi wake
wanaojitegemea.
“Divisheni Maalumu ya Mahakama Kuu, itakuwa
na majaji pamoja na watumishi wengine, ambao
wanahusika moja kwa moja na kesi za rushwa
na uhujumu uchumi tu. “Hatua hii itawezesha
kesi za makosa ya rushwa na uhujumu uchumi
kusikilizwa kwa urahisi, ufanisi na kwa haraka,”
alisema Masaju wakati alipokuwa akisoma
muswada huo kabla ya kupitishwa na Bunge.
Hatua hiyo ya kuwa na majaji maalumu na
wafanyakazi wake, Masaju alisema imelenga
kuondoa udhaifu uliojitokeza wakati wa
kushughulikia kesi za rushwa na uhujumu
uchumi, kwa kuwa majaji waliokuwa wakisikiliza
mashauri hayo, walikuwa hao hao wanaosikiliza
mashauri mengine ya jinai, madai, katiba na
mengine yanayofunguliwa Mahakama Kuu.
Kwa mujibu wa Masaju, hali hiyo ilisababisha
uendeshaji wa kesi za rushwa na uhujumu
uchumi, kutokuwa na tofauti na uendeshaji na
usikilizwaji wa kesi zingine. Mazingira mengine
wezeshi yanayotengenezwa na sheria hiyo kwa
divisheni hiyo, ni thamani ya fedha
inayohusishwa na makosa hayo, kuwa inaanzia
Sh bilioni moja.
“Inapendekezwa kuwa pale makosa ya rushwa na
uhujumu uchumi yanapohusisha thamani ya
fedha, basi makosa yatakayofunguliwa katika
Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na
Uhujumu Uchumi, yawe ni yale ambayo thamani
yake haipungui Sh bilioni moja,” alisema
Masaju.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top