Mahakama ya ICC imemhukum Pieere Bemba kwenda jela miaka 18.doma zaid.
Majaji katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu
ICC wamemhukumu makamu wa zamani wa rais
katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Jean-
Pierre Bemba, kwenda jela miaka 18 kwa
kuhusika katika ubakaji wa kinyama na mauaji
katika Jamuri ya Afrika ya Kati muongo mmoja
uliopita. Bemba alishindwa kulidhibiti jeshi lake la
binafsi ambalo alilituma kwenda nchini Jamhuri
ya Afrika ya Kati mnamo Oktoba 2002 ambako
walifanya vitendo vya kikatili vya ubakaji, mauaji
na uporaji wa kikatili.chanzo DW Swahili.
0 comments :
Post a Comment