Mbunge aangua kilio kisa bajet ya sekta ya Afya nindogo.soma zaid
MWAKILISHI wa Jimbo la Paje, Jaku Hashim
Ayoub jana aliangua kilio ndani ya Baraza la
Wawakilishi akilalamika bajeti ndogo iliyotengwa
na serikali katika sekta ya afya.
Ayoub alisema wananchi wa Zanzibar
wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ya afya
kutokana na bajeti ndogo inayotengwa na serikali
na hivyo kulazimika kuchangia huduma hizo, licha
ya kutangazwa kuwa bure.
Alitoa mfano kuwa, huduma za kujifungua
zimetangazwa bure na Rais wa Zanzibar, Dk Ali
Mohamed Shein, lakini kutokana na bajeti ndogo
iliyotengwa kuhudumia sekta hiyo, wazazi
wanalazimika kuchangia.
“Mheshimiwa Mwenyekiti siungi mkono bajeti hii
na nawaomba wenzangu kufanya hivyo kwa
sababu fedha zilizotengwa kwa ajili ya kutoa
huduma za afya kwa wananchi ni ndogo sana,”
alisema.
Alisema wizara imetangaza rasmi kwamba sasa
Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja, lakini kwa
bahati mbaya haina uwezo wa kutoa huduma
muhimu za afya, ikiwemo vifaa vya kupiga picha
za wagonjwa.
Alisema katika bajeti ya Wizara ya Afya huduma
katika Hospitali ya Mnazi Mmoja zimetengwa
jumla ya Sh bilioni 7.5 ambazo ni kidogo sana
kwa hospitali ambayo imepandishwa hadhi na
kuwa hospitali ya rufaa.
Baadhi ya Wawakilishi wa Pemba wameipongeza
Serikali ya Mapinduzi (SMZ) kwa juhudi zake
katika kuifanyia ukarabati mkubwa Hospitali ya
Abdalla Mzee iliyopo Pemba. Mwakilishi Bahati
Khamis Kombo alisema hatua hiyo itawapunguzia
usumbufu uliokuwepo awali kwa wananchi wa
Pemba kufunga safari hadi Unguja kutafuta
matibabu au kwenda Tanzania Bara.
“Tumefurahishwa na juhudi za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar ya kuifanyia ukarabati
mkubwa Hospitali ya Abdallah Mzee iliyopo
Pemba ambayo itakapomalizika itakuwa na hadhi
ya hospitali ya rufaa kwa kutoa huduma katika
maeneo yote muhimu ya afya,” alisema.
Akisoma maoni ya Kamati ya Maendeleo ya
Ustawi wa Jamii, Mwenyekiti wake, Dk
Mwinyihaji Makame Mwadini alisema bajeti
ndogo iliyotengwa na serikali katika sekta afya
itashindwa kutekeleza malengo muhimu ya
kupambana na maradhi hatari. Wizara ya Afya
imeomba kuidhinishiwa Sh 59,228,631,000 kwa
mwaka wa fedha 2016/2017.chanzo habar Leo.
0 comments :
Post a Comment