Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, June 21, 2016

Serikali yafuta kodi kwa taasisi za Dini kwa bidhaa wanazozinunua.soma zaid.


Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip mpango
amesema amefuta utaratibu alioupendekeza
bungeni wa taasisi za dini kulazimika kulipa kodi
kwanza kwa bidhaa watakazonunua au kuagiza
nje na kodi hiyo kurejeshwa baada ya ukaguzi
kufanyika.
Waziri Mpango ameyasema hayo leo alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa
akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja za wabunge
kuhusu Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa
fedha 2016/2017.
Amesema kwa kutambua mchango mkubwa wa
taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji huduma
za elimu na afya anapendekeza kufuta utaratibu
huo na badala yake Serikali itaimarisha zaidi
hatua mbalimbali za udhibiti wa msamaha ya
kodi.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top