Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, June 26, 2016

Ukawa kutoshiriki mikutano inayomhusu Rais magufuli.soma zaid.

Uongozi wa CHADEMA kanda maalum ya Pwani kwa kushirikiana na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, umewataka madiwani na mameya wote ndani ya Dar es Salaam kutoshiriki mikutano itakayomhusu Rais Dkt John Magufuli kwa kile wanachodai kuwa serikali imekuwa haiwapi ushirikiano hata katika masuala ya msingi ya kimaendeleo. Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari imetolewa na katibu wa kanda hiyo ya Pwani Bw Casmir Mabina, ambapo pamoja na masuala mengine taarifa hiyo imesema wanapinga ukandamizwaji wa demokrasia unaoenda kinyume na katiba ya nchi na ile ya vyama vya siasa ya mwaka 1992. Mwenyekiti wa kanda hiyo Mwita Witara na mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Ilala Dkt Makongoro Mahanga wamesema bado viongozi wa upinzani katika manispaa za jiji wamekuwa wakinyimwa uhuru wa kufanya kazi zao. Katika hatua nyingine meya wa jiji la Dar es Salaam ameunga hatua mpya ya kupambana na madawa ya kulevya ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakiwaathiri vijana na kupoteza nguvu kazi ya Taifa, huku pia akiwataka vijana kujiepusha na matumizi ya dawa hizo.chanzo ITV.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top