Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, June 26, 2016

Wilaya ya kishavu huenda isifikie leo hili.soma zaid.

Halmashuri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga huenda isifikie lengo la kukamilisha zoezi la utengenezaji wa Madawati hadi ifikapo tarehe ya mwisho iliyoagizwa na Mh.Rais John Pombe Magufuli hali ambayo imetajwa kuwa imesababishwa na uhaba wa vyanzo vya mapato na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyosababisha baadhi ya mazao ya biashara kushindwa kustawi na kuikosesha halmashauri mapato ya ndani. Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Kishapu Bi.Hawa Ng’umbi wakati akipokea madawati 1,000 kati ya madawati 2,600 yaliyochangiwa na mgodi wa Almasi wa Wiliamson Diamond idadi ambayo inakamilisha asilimia sitini tu ya madawati yanayohitajika katika shule za msingi na sekondari wilayani humo. Aidha meneja mkuu wa mgodi wa almasi wa Wiliamson Diamond Bw.Arlen Loehmar amesema mbali na kuchangia idadi hiyo ya madawati mgodi utaendelea kuisaidia jamii katika miradi mbalimbali ya maendeleo hali ambayo imekuwa ikijenga mahusiano mazuri na jamii inayouzunguka mgodi. Kwa upande wao baadhi ya wazazi walioshiriki katika zoezi hilo wamewataka wazazi wengine kujitokeza kuchangia zoezi la ukamilishaji wa madawati lakini pia wameyataka makampuni mengine,watu binafsi na mashirika mbalimbali kuunga mkono jitihada za mh.john pombe magufuli katika kuimarisha elimu.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top