Watumishi kubandikwa majina watakaolipwa mishahara wilayani kahama.soma zaid.
Mkuu wa wilaya Kahama Vitta Kawawa
amewaagiza maofisa watumishi katika
halmashauri tatu zinazounda wilaya hiyo
kubandika majina ya watumishi watakaolipwa
mishahara kila mwisho wa mwezi na watumishi
kuhakiki majina yao na watakapobaini majina ya
watumishi ambao hawapo kazini watoe taarifa
mara moja ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Mfumo huo mpya unaolenga kuendelea kubaini
watumishi hewa umetangazwa na Mkuu wa
wilaya ya Kahama Bw.Vitta Kawawa wakati
akipokea miradi ya maendeleo ya elimu kutoka
katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu
unaomilikiwa na kampuni ya Acacia miradi
iliyotekelezwa kwa thamani zaidi ya shilingi
milioni 279.
Akikabidhi miradi hiyo ambayo ni
madawati,nyumba za walimu,vyoo vya
wanafunzi,pikipiki na majengo ya shule ya
sekondari Bugarama yaliyokarabatiwa,Kaimu
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu Bw.Benedict Busunzu,amesema
kampuni ya Acacia imejikita katika kusaidia sekta
ya elimu ili kuiwezesha serikali kuzalisha
wataalamu,watakaoliwezesha taifa kuingia katika
soko la ushindani wa ajira duniani.
Baadhi ya waalimu wa shule za msingi na
sekondari wilayani humo wamedai kuwa
kumekuwepo na idadi kubwa ya wafanyakazi
hewa ambao nao walijitokeza kuhakikiwa ambapo
zoezi la kubandika majina ya watumishi litasaidia
kuwabaini.
kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa baada ya
zoezi la uhakiki wa wafanyakazi katika wilaya ya
kahama,inasemekana shilingi milioni 360 ambazo
zingeweza kutatua kero mbalimbali za wananchi
zimetumika kulipa wafanyakazi hewa.chanzo itv
0 comments :
Post a Comment